Breaking News

Nusrat Jahan Rafi: Hukumu ya kifo kwa watu 16 waliomchoma moto mwanafunzi Bangladesh


Picha ya Nusrat Jahan RafiHaki miliki ya pichaFAMILY HANDOUT
Image captionNusrat alimwagiliwa mafuta ya taa na kuchomwa moto juu ya paa
Mahakama nchini Bangladesh imewahukumu kifo watu 16 waliomchoma moto hadi kufa mwanafunzi kwa kuripoti kuwa mwalimu mkuu amenyanyasa kingono.
Nusrat Jahan Rafi, 19, alifariki mwezi Aprili katika mji wa Feni, uliopo kilo mita 160 nje ya mji mkuu wa Dhaka.
Mwalimu mkuu aliyetuhumiwa na Nusrat kwa unyanyasaji na wanafunzi wawili wa kike ni miongoni mwa waliohukumiwa kifo.
Kifo chake kilishangaza nchi nzima na kusababisha msururu wa maandamano kushinikiza Nusrat apate haki.
Kesi hiyo ni ya kwanza kuamuliwa haraka nchini ikilinganishwa na nyingine kama hizo ambazo huchukua miaka kadhaa kabla ya kuamuliwa. Mwendesha mashtaka Hafez Ahmed aliwaambia wanahabari kuwa "wauaji sharti wachukuliwe hatua Bangladesh".
Mawakili wa washtakiwa wanasema watakata rufaa.

No comments