KAZI YA MKE WANGU YANIFANYA KUTOPATA WATOTO AU HATA PENZI NDANI YA NDOA.
"Rasmi 14/09/2021 ndoa yangu imetimiza miaka miaka nne,nikiwa nimemuoa mwanamke ambaye siku zote niliamini ni mwanamke wa ndoto zangu na niliamini kuwa ndie mwanamke pekee atakae nipa furaha maishani mwangu"
lakini naweza kukiri kwangu hii ni ndoa ambayo najuta kuoa,nakosa furaha ndani ya ndoa,na ukwei ni ndoa ambayo imenifanya NICHUKIE na kujiisi nilipoteza muda wangu.Kazi ya mke wangu,imekuwa ndio mume wake na ndio imekuwa starehe kubwa kwake,na anaithamini hata kuliko mimi ambae nilipiga goti na kumuuliza "Baby,will you marry me?" na kwa tabasamu akaitikia na kusema "Yes,Fidel...i will marry you my love"
Najiuliza Fidel nilikosea wapi,kuruhusu mke wangu afanye kazi au kosa gani kubwa nimefanya.kiufupi ni mwaka wa nne sasa,mtoto hatuna kwa ndoa,sababu si kwamba sote tuna matatizo,hapana ni kwamba yupo 'busy' hadi m,uda wa kufanya tendo la ndoa hana kabisa.
kwenye ndoa nilipata mapenzi miezi mitano ya mwanzo baada ya kupta kazi ambayo anatoka asubui na anarudi usiku kila siku imekuwa kaa la moto.Nimemuomba aache kazi nimfungulie biashara,amekataa kata kata ,akirudi kutoka kazini anadai amechoka sana hadi kupika inabidi niingie jikoni mimi ili nipike ndio tuweze kula.
Ni ukweli kwamba hadi sasa sijui nifanye nini ila hii ndoa kwangu haina furaha na chanzo ni kazi ya mke wangu,ambayo mke wangu amegoma kabisa kuacha.mpka sasa ni mwaka wa nne na dalili za kuitwa baba na hata furaha na amani ya ndoa sina kabisa.maana hata penzi tu sipewi na nikilazimisha nasusiwa kama mzoga,ukweli haya maisha ya ndoa kwangu yamekuwa magumu
Imefikia hatua natamani hata kuwa n amwanamke mwengine wa pembeni.ila sipendi kuwa msaliti ila pia nikijiangalia naona kabisa siwezi simama mbele ya wantu na kusema nina ndoa ya kujivunia.Nina uhakika kabisa ndoa yetu ipo kwenye makaratasi tu,ila kwa matendo tu mimi niko single tean yule wa kiwango cha juu...
TAFADHALINI NAOMBA USHAURI WENU....
No comments