HARUFU YA UFISADI KUHUSUHU FEDHA ZA COVI-19 NCHINI KENYA
Kamati ya bunge inayosim,amamia hesabu za bunge nchini kenya imetoa siku 60 kwa mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikaali kufanya ukaguzi wa kina kwenye mamlaka ya usabazaji wa dawa nchini humo baada ya kutilia shaka matumizi ya mabilioni ya fedha za kupambana na ugonjwa wa covid-19.
spika wa bunge la taifa la Kenya,mheshimiwa Justin Muturi amesema kuwa bunge hilo litashiriki kikamilifu na ipasavyo katika kuhakikisha kuwa fedha zilizotengwa kwajili ya kupambana na covid-19 zimetumika ipasavyo,na wabadhirifu wanawajibishwa.
Kamati iyo ya bunge imeeleza kuwa,inataka maelezo ya kina na kupewa taarifa za mara kwa mara jinsi fedha izo matumizi ya mabilioni hayo yanavyotumika kusaidia wakenya.
''Tunatoa ukomo wa siku 60 kwanzia leo ilitupate taarifa kamili kuhusu ukaguzi ...ndani ya mwezi mmoja tu,tunatarajia kupata ripoti ya awali'' mwenyekiti wa kamati iyo,ambae pia ni mbunge wa Ugunja,Opiyo Wandayi amekarieriwa na Citizen Tv. Kamati hiyo imeekeleza uchunguzi huo uangazie pia tuhuma za rushwa na ufisadi na kuhakikisha kuwa wakenya wanafahamu ukweli.
No comments